15 Mei 2014 - 22:04
Homa ya Dengue

Virusi vya homa ya dengue vinaenezwa kwa binadamu baada ya kuumwa na mbu aina ya “Aedes”. Mbu hawa hupendelea kuzaliana kwenye maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu au hata ndani ya nyumba. Viluwiluwi vya mbu hawa huweza kuishi katika mazingara ya ndani ya nyumba mpaka wakawa mbu kamili na kuanza kusambaza ugonjwa huu kwa binadamu. Mbu hawa huwa na tabia ya kuuma wakati wa mchana.

Homa ya dengue ni ugonjwa unaosababishwa na kirusi ambacho kinaenezwa na mbu wa aina ya Aedes. 
Virusi vya homa ya dengue vinaenezwa kwa binadamu baada ya kuumwa na mbu aina ya “Aedes”. Mbu hawa hupendelea kuzaliana kwenye maji yaliyotuama karibu na makazi ya watu au hata ndani ya nyumba. Viluwiluwi vya mbu hawa huweza kuishi katika mazingara ya ndani ya nyumba mpaka wakawa mbu kamili na kuanza kusambaza ugonjwa huu kwa binadamu. Mbu hawa huwa na tabia ya kuuma wakati wa mchana.
Dalili za ungonjwa huu:
Homa kali naya ghafla,Kichwa kuuma sana,Macho kuuma,Maumivu makali ya misuli naviungo,Kutapika,Kutokwa damu hasa puani, na Kichefuchefu.
Tahadhari:
Wakati mwingine dalili za ugonjwa huu zinaweza kufanana sana na dalili za malaria, hivyo basi wananchi wanaombwa kuwa makini na kuhakikisha wanapima ili kugundua kama wana vimelea vya malaria ua Dengue ili kupata matibabu yanayostahiki.
Kinga ya ungonjwa huu:
Jinsi ya kujikinga na ugonjwa wa homa ya dengue
:Kuangamiza mazalio ya mbu 
- Fukia madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo
- Ondoa vitu vyote vinavyoweza kuweka mazalio ya mbu kama vile, vifuu vya nazi, makopo, magurudumu ya magari yaliyotupwa hovyo, nk.
- Fyeka vichaka vilivyo karibu na makazi ya watu
- Hakikisha maua yandayopandwa kwenye makopo au ndoo hayaruhusu maji kutuama
- Funika mashimo ya maji taka kwa mfuniko imara
- Safisha gata za paa la nyumba ili kutoruhusu maji kutuama
:Kujikinga na kuumwa na mbu 
- Kumia dawa za kufukuza mbu “mosquito repellants”
- Vaa nguo ndefu kujikinga na kuumwa na mbu
- Tumia vyandarua vyenye viuatilifu (hata kwa wale wanaolala majira ya mchana)
-Weka nyavu kwenye madirisha na milango ya nyumba za kuishi
Huduma ya kwanza:
1. Tumia oral yaani nunua pakti ya oral (chumvi na sukari) mpe mgonjwa anywe. Hii ni kurudishia maji yaliyopotea kwa kutapika na homa kali.
2. Mpe Panadol au paracetamol
3. USIMPE MGONJWA ASPIRINI HIYO NI HATARI KWANI ITACHOCHEA INTERNAL BLEEDING

Hitimisho

Wananchi wanashauriwa kutokuwa na hofu kuhusu ugonjwa huu bali wanashauriwa kwenda katika vituo vya tiba mara mnapoona dalili.